MWINGILIANOTANZU KATIKA UAINISHAJI WA TANZU ZA FASIHI SIMULIZI YA KISWAHILI.
Abstract
Makala hii imejikita katika kujadili mwingilianotanzu katika uainishaji wa tanzu za fasihi
simulizi ya Kiswahili. Mwingilianotanzu hurejelea namna utanzu ulivyotagusana na tanzu
zingine na matini yote kwa ujumla ili kuboresha uwasilishaji wa ujumbe. Kama anavyosema
Mulokozi (1989), hakuna utanzu wowote ule uliojitosheleza ila tanzu huingiliana na matumizi ya
tanzu zingine ili kufaulisha uwasilishaji wa ujumbe. Mwingilianotanzu hutumiwa na mwandishi
kwa kujua au kwa kutojua. Dhana ya mwingilianotanzu inaondoa mipaka ya kazi husika na
kuiweka wazi kutazamwa kwa kuzingatia jinsi ilivyojumuisha mitindo na mbinu mbalimbali kwa
mfumo uliosukwa taratibu ili kuwasilisha ujumbe wake. Wamitila (2008) anadahili kuwa
mwingilianotanzu katika kazi moja hutoa nafasi kubwa ya msanii kujieleza barabara.
Downloads
Author(s) and co-author(s) jointly and severally represent and warrant that the Article is original with the author(s) and does not infringe any copyright or violate any other right of any third parties, and that the Article has not been published elsewhere. Author(s) agree to the terms that the IJRDO Journal will have the full right to remove the published article on any misconduct found in the published article.